Viscud Mtarishi kijana mwenye uchungu na jimbo la mikumi, atoa somo kwa vijana wote wa mikumi soma hapa

https://fbcdn-sphotos-f-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xpa1/v/t1.0-9/10487203_712880745491703_9023421984054506188_n.jpg?oh=fb53c25be14e92373c5f71d8d60636f9&oe=554BBEBA&__gda__=1431766530_7ee2777568f77a172981c83752daf6f9 

Uchama tuweke pembeni,wanaomkubali Joseph Haule ni wale ambao hawajawaona wala kuwasikia watia nia wengine jimboni mikumi.Yupo Dr makweta pia halafu huyo kijana Hasheem ambaye kwangu mimi ni classmate.Mikumi ina watu makini mno,mikumi ina vijana wenye upeo mkubwa mno na jimbo lenyewe ni tajiri mno isipokuwa rasilimali zote bado ni ghafi.
Hasheem ana kikao muhimu kabisa cha kiuongozi na kiutawala kazini singida na yeye kama mhifadhi lazima aondoke kesho kurejea kibaruani.Sasa game itakuwa tamu sana kwani tumeomba kituo kimoja cha redio mkoani morogoro kutuandalia Dak.120 ili vijana watia nia wote wa mikumi wapate nafasi hata ya dak kumi kumi tu kujitambulisha kwa wanamikumi na nini mipango yao kwa mikumi na siyo kupitapita tu huko vjjn na yoyoyoyoyo.Tunataka mikumi ya kisasa na mikumi ya kisayansi,tumataka mikumi inayokimbia kwani tumechoka kutembea na tunataka mikumi inayowavutia vijana wake kuwekeza mikumi na siyo mikumi hii inayowakimbiza vijana.Itikadi za kisiasa kwa sasa siyo mkombozi tena wajimbo.Tunataka mtu na hatutaki chama hata kidogo.Mikumi tuitakayo tutaipata tena mapema sana kama tutakuwa pamoja.MUNGU IBARIKI MIKUMI YETU



No comments:

Post a Comment

Translate

 
Support : Admin Mikumi Yetu Mikumi Yetu
Copyright © 2009. MIKUMI YETU - Haki Zote Zimehifadhiwa.
Sponsored by MIKUMI YETU
Proudly powered by MIKUMI YETU